Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amezindua uwanja wa ndege katika kambi ya kijeshi ya anga iliyoko Ngerengere mkoani Morogoro ambapo alisema anajivunia kutoka madarakani akiwa ameiacha nchi katika hali nzuri ya kiusalama. Rais Kikwete akizungumza katika uzinduzi huo alisema katika kipindi cha uongozi wake amefanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuliacha jeshi likiwa katika hali nzuri ambapo alieleza hakuna nchi inayoweza kuwa na maendeleo kama haina jeshi imara. Kwa upande wake mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuliimarisha jeshi la Tanzania ingawa zipo changamoto ndogodogo lakini anaamini serikali itazifanyia kazi ili kuweza kuwa na jeshi imara. Tazama Video Ya Ufunguzi Huo Hapo Chini
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat