Licha ya hatua ya serikari kuyachepua masoko ya fedha katika siku za hivi karibuni, hali ya wasiwasi imezuka kwa wawekezaji nchini China kutokana na kushuka kwa hisa kwa masoko ya fedha nchini humo. Soko kuu la hisa la Shanghai lilifunga biashara yake kwa bei iliyopungua kwa asilimia sita. Kampuni za serikali ya nchi ya China zimekuwa zikinunua hisa ili kuimarisha bei na serikali imesema inachunguza madai ya kuchezea bei ya hisa na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwani hali inavyoelekea upo uwezekano wa kupungua wawekezaji ambao ni zaidi ya asilimia 90. FOLLOW INSTAGRAM@sosteneslekule
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat