Quantcast
Channel: AutomobileHeat » electronics
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1695

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Apiga Marufuku Kuuza na Kunywa Pombe Saa za Kazi

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi. Amri hiyo ameitoa jana katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari. Gallawa alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 61, Ibara ndogo ya 4.    Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni. Aidha mkuu huyo wa mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kusimamia utekelezaji wa amri hiyo na kuongeza kuwa yoyote atakayekiuka amri hiyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1695

Trending Articles