Wakati Lipumba akiwaambia waandishi wa habari jana kwamba kadi yake ya uanachama bado iko hai hadi mwaka 2020, akimaanisha kuwa ataendelea kuwa mwanachama wa CUF nje ya uongozi, taarifa zilizotufikia zinasema kuwa chama hicho kinajiandaa kumfukuza. Katika sehemu ya taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa habari, Uenezi na Umma wa CUF,Ismai Jussa, inasomeka; “….Katibu Mkuu ameagiza kuitishwa vikao vya dharura vya kamati ya utendaji ya taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa Jumapili, Agosti 9 2015,kujadili hatua hiyo na kufanya uamuzi juu ya hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki.” Mpekuzi imedokezwa kuwa miongni mwa uamuzi unaotarajiwa kufikiwa kesho na vikao hivyo ni kumfukuza ndani ya chama hicho Profesa Lipumba.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat