Quantcast
Channel: AutomobileHeat » electronics
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1695

Rais Kikwete aifariji familia ya marehemu mzee Peter Kisumo

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo Upanga jijini Dar es salaam alipokwenda kwenye msiba wa mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo,  aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya Figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa wanasiasa  wakongwe nchini, Marehemu Mzee Peter Kisumo,  aliyefariki dunia Jumatatu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya Figo. Marehemu Mzee Kisumo alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhamini wa Chama cha CCM na aliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri. (Picha na IKULU).

[via LEKULE]

Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1695

Trending Articles