Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery. MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya vizuri, Malaika Exavery amesema anakerwa na kitendo cha watu wengi kumfananisha na muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’. Akizungumza na LEKULE, Malaika alisema huko nyuma alipokuwa akifananishwa na msanii huyo hakujali, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda imekuwa ni shida hadi wengine wanamsimamisha. “Unajua kufananishwa na mtu siyo tatizo, lakini kwa hali ilivyo hivi sasa lazima mtu usikie kuchoka kabisa kwa sababu hata wakati mwingine unaendesha gari mtu anakusi mamisha halafu akikuangalia usoni vizuri anaondoka, anasema alidhani ni Lulu,” alisema Malaika.
[via LEKULE]
Follow us @automobileheat – lists / @sectorheat